Watakatifu Tisa walikuwa wamisionari waliochangia sana ustawi wa Ukristo katika Ethiopia ya leo mwishoni mwa karne ya 5. Majina yao ni: Abba Aftse, Abba Alef, Abba Aragawi, Abba Garima (Isaka), Abba Guba, Abba Liqanos, Abba Panteleoni, Abba Sehma na Abba Yemata.
Ingawa wanasemekana kutokea Syria, ukweli ni kwamba wawili au watatu tu walitokea huko; wengine walitokea Konstantinopoli, Anatolia, na hata Roma.[1] Mwanahistoria Tadesse Tamrat anasema walikimbilia Ethiopia ili kukwepa dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia.
Kabla yao Ukristo ulikuwa umeishia katika sehemu nyembamba kati ya Adulis na Aksum kwenye njia za misafara[2]
Pamoja na kuongoa wananchi, walianzisha pia idadi ya monasteri zilizopewa kanuni ya Pakomi: Abba Aftse alianzisha ile ya Yeha; Abba Alef ile ya Bi'isa karibu na Mto Mareb; Abba Aragawi ile muhimu ya Debre Damo; Abba Likano na Panteleoni ile ya Axum; Abba Garima nyingine kaskazini kwa Adwa[3][4]; Abba Guba ile ya Madara; Abba Sehma ile ya Sedenya; na Abba Yem’ata ile ya Gar'alta.[5]
Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[6]
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search